>

SIMBA YANYOOSHWA UWANJA WA KAITABA

Uwanja wa Kaitaba dakika 90 zimekamilika mbinu ya Pablo Franco imekwama mbele ya Kagera Sugar.

Ni Hamis Kiiza dakika ya 70 aliwatungua Simba baada ya safu ya ulinzi kufanya makosa katika kuokoa shambulizi la kushtukiza.

Hakuna sababu nyingine kwa Franco ambaye alikuwa kwenye uwanja mzuri wa kapeti wa Kaitaba kakwama kushinda ugenini.

Simba inabaki na pointi zake 25 ikiwa imecheza mechi 13 na vinara ni Yanga wenye pointi 35.

Kiiza alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano Ikumbukwe kwamba Kiiza amewahi kucheza ndani ya Simba na kwa sasa ni ingizo jipya ndani ya Kagera Sugar.

Huu ni mchezo wa pili kwa Simba kupoteza baada ya ule wa kwanza kuwa mbele ya Mbeya City na bao walilofungwa ni moja.

Hakuna kiporo kwa sasa na ni tofauti ya pointi 10 kati ya Simba na Yanga ambao ni vinara wa ligi.