KLOPP ANAAMINI MARTINELL ATAKUJA KUWA TISHIO

KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anaamini kwamba nyota wa Arsenal, Gabriel Martinelli atakuja kuwa tishio baadaye ikiwa ataendelea kuwa kwenye mwendo mzuri.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba atakuja kufanya vizuri pia ikiwa hatapata majeraha kwa kuwa ikiwa hivyo itakuwa shida kwake kuweza kucheza katika ubora ambao ameanza nao.

Raia huyo wa Brazil ameanza vema ndani ya Arsenal lakini msimu uliopita wote alikuwa nje akitibu majeraha ambayo yaliweza kupunguza kasi yake.

Klopp amesema:”Martinell ni mchezaji ambaye huko mbele ya safari tutamzungumzia sana na mtakuja kuniambia.

“Kama asingekuwa na majeraha basi kwa sasa angekuwa ni tishio kwani anawafanya mabeki wawe bize muda wote kutokana na kasi yake pamoja na mbinu zake, yeye ni mchezaji aliyekamilika,”.