>

HAJI MANARA:TUKAE WIKI TANGA TUFUNGWE?

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa isingekuwa rahisi kwa Yanga kufungwa kwenye mchezo wao wa jana kwa kuwa walijipanga kushinda na walitumia muda mwingi wakiwa Tanga.

Januari 16 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 0-2 Yanga na kuwafanua waweze kusepa na pointi tatu mazima ambapo mabao yalifungwa na Said Ntibanzokiza kwa pasi ya Khalid Aucho na Fiston Mayele aliyetumia pasi ya Ntibanzokiza.

Manara amesema:”Yaani sisi tukae hapa wiki halafu tufungwe na Coastal Union kweli haiwezekanihaiwezekani, tumejipanga na tumeshinda. Tunawashukuru mashabiki wetu waliokuwa hapa Tanga waliotoka sehemu mbalimbali lakini tunafurahi.

“Dhamira yetu ilikuwa ni kushinda hivyo haijalishi tulikuwa tunafanyaje,walitamba sana waliongea sana wakatuchukulia mazoea wakadhani hii Yanga unaweza kuizoea hii haiwezekani.

“Tulikuwa tumejipanga kupata pointi tatu haijalishi namna gani muda gani tunaweza kufanya, tunaondoka na pointi tatu tunaangalia mechi yetu ijayo,” amesema.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 12 ndani ya Ligi Kuu Bara.