MBEYA CITY:TUMEJIANDAA KUPATA POINTI KWA SIMBA

KUELEKEA mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba, benchi la ufundi la Mbeya City limetamba kuwa licha ya ubora walionao wapinzani wao lakini watahakikisha wanapata ushindi.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Januari 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Meneja wa Mbeya City, Mwegane Yeya, amesema: “Tunaendelea na maandalizi kuelekea kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya Simba.

“Tunajua Simba wana timu nzuri, wachezaji wazuri kutokana na ubora waliouonyesha kwenye michuano ya Mapinduzi lakini hata sisi pia tuna kikosi bora, hivyo tutahakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Utakuwa mchezo mgumu lakini sisi haitutishi, tutahakikisha tunautumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kwa kupata pointi tatu kama ikishindikana basi tupate pointi moja kuliko kupoteza.”