>

YANGA YAIPELEKEA MZIKI MNENE COASTAL UNION

KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Kikosi cha Yanga kimerejea kambini jana Jumatano ambapo uongozi umefunguka kuwa utaenda kucheza mchezo huo wakiwa na kikosi kamili ili kujihakikishia ubingwa.


Yanga ilirejea Dar
juzi Jumanne ikitokea Zanzibar baada ya kutolewa hatua ya nusu fainali ya Kombe la
Mapinduzi dhidi ya Azam
FC.


Akizungumza na
Spoti Xtra, Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro, alisema kuwa: “Tunamshukuru Mungu timu imerejea salama kutoka Zanzibar na imeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa
ligi dhidi ya Coastal Union.


“Tunajua utakuwa
mchezo mgumu kwa upande wetu, lakini tunajipanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri
kwani kilichotokea Zanzibar
ilikuwa bahati mbaya.

 

“Baada ya likizo ya muda mfupi ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi anatarajia kurejea nchini leo (jana) na kikosi kitaondoka Dar Ijumaa (kesho) kuelekea Tanga kwenye mchezo huo.”