SIMBA WATAJA SIKU YA KUMPOKEA CHAMA

UONGOZI wa Simba SC, umepanga kumtambulisha Clatous Chama siku ya mwisho kabla ya usajili wa dirisha dogo haujafungwa Januari 15, mwaka huu.


Chama ambaye aliitumikia
Simba kwa misimu mitatu, aliondoka kikosini hapo mwishoni mwa msimu wa
2020/21 na kutimkia RS
Berkane ya Morocco.


Kwa muda mrefu, kumekuwa
na tetesi za Simba kuhitaji kumrudisha kundini kiungo huyo wa Zambia ambaye
inasemekana hana furaha ndani
ya RS Berkane.


Chanzo kutoka katika
kambi ya Simba iliyopo Zanzibar, kimeliambia Spoti Xtra kwamba: “Chama ameshamalizana na viongozi na muda si mrefu tutampokea Dar, hii ni baada ya kumaliza majukumu yetu ya Kombe la
Mapinduzi.


“Baada ya kumpokea
Chama, viongozi wamepanga kumtambulisha siku ya mwisho kabisa ya usajili.” Kwa upande wa Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia ishu hiyo akisema:

 

“Baada ya Kombe la Mapinduzi, tukutane Uwanja wa Julius Nyerere jijini Dar, tuna jambo letu. Siwezi kusema moja kwa moja ni Chama, ila mashabiki wa Simba watafurahi sana.”