>

FAINALI DUME,DAKIKA 45 AZAM FC 0-0 SIMBA

NGOMA kwa sasa ni mapumziko mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC dhidi ya Simba, Uwanja wa Amaan.

Dakika 45 zimekamilika kwa timu zote kukamilisha ngwe ya kwanza bila kuweza kufungana.

Ni bonge moja ya mchezo umechezwa Uwanja wa Amaan ambapo timu zote zinaonesha kwamba zinasaka Kombe la Mapinduzi.

Hakuna kadi ya njano wala nyekundu ambayo imeonyeshwa mpaka sasa licha ya migongano ya hapa na pale kuwepo ndani ya uwanja.

Nyota wa zamani wa Simba, Ibrahim Ajibu ameanza kuonyesha makeke yake mbele ya mabosi wake wa zamani Simba huku Simba wao wakiwa na kikosi kilekile kilichaonza dhidi ya Namungo FC.