>

PABLO ALITAKA KOMBE LA MAPINDUZI

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanahitaji kulitwaa Kombe la Mapinduzi hivyo leo watapambana kupata matokeo mbele ya Namungo FC.

Saa 2:15 usiku Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Azam FC ama Yanga ambao ni mabingwa watetezi.

Kocha huyo amesema:”Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi ambazo tutacheza na ikiwa tutashinda maana yake tunaongeza nafasi ya kuweza kutwaa Kombe la Mapinduzi.

“Tunahitaji ubingwa mabadiliko kwenye mchezo wetu ambao umepita ulikuwa na sababu maalumu za kuwalinda wachezaji na kuwaepusha na majeraha, Wanasimba wasiwe na mashaka tupo tayari,”.