NI SIMBA V AZAM FC FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

USHINDI wa mabao 2-0  walioupata Simba leo Januari 10 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan katika Kombe la Mapinduzi unawafanya waweze kutinga hatua ya fainali.

Ni mabao ya Meddie Kagere dakika ya 14 na PapeSakho dakika ya 48 yametosha kuwapa ushindi Simba.

Sasa Simba itakutana na Azam FC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi Januari 13.

Azam FC ilishinda kwenye mchezo wa fainali ya kwanza dhidi ya Yanga na ilishinda kwa penalti 9-8.

Mchezaji bora wa mchezo wa leo amechaguliwa kuwa Sakho na amekabidhiwa zawadi ya milioni moja.

Frank Mangingi wa Namungo yeye amekabidhiwa tuzo ya mchezaji muungwana na amekabidhiwa laki tatu.