>

DAKIKA 45,SIMBA 1-0 NAMUNGO FC

SIMBA inakwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa kufunga bao 1-0 dhidi ya Namungo FC baada ya dakika 45 kukamilika.

Ni Meddie Kagere amepachika bao la kuongoza katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Namungo FC.

Bao hilo limepachikwa dakika ya 14 baada ya kipa wa Namungo, kutema mpira uliopigwa na Sakho.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na Azam FC iliyoweza kushinda katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Yanga.