JEREMIA Kisubi, kipa namba tatu wa Simba leo Januari 10,2022 ametambulishwa ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar.
Usajili wake ni wa mkopo akitokea Simba ambapo huko alikuwa hapati nafasi ya kuanza katika mechi za ushindani.
Aliibuka ndani ya Simba akitokea Tanzania Prisons ambapo huko alikuwa ni chaguo namba moja la benchi la ufundi.
Ni nafasi ya Aboutwalib Mshery ambayo kwa sasa ni mali ya Yanga anakwenda kuichukua.