AZAM FC YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

MABINGWA wa kihistoria kwenye Kombe la Mapinduzi, Azam FC leo wameibuka na ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mbele ya Yanga kwa ushindi wa penalti.

Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu hivyo mshindi ametafutwa kwa kupitia mikwaju ya penalti.

Ilikuwa ni moja ya mchezo wenye ushindani mkubwa ambapo Azam FC wao waliweza kupachika penalti 9 kimiani huku Yanga ikifunga penalti 8.

Zile tano tano za mwanzo zilikamilika kwa kila timu kufunga jambo lililopelekea kuweza kuanza kupigiana penalti mojamoja.

Ngoma ilikuwa nzito kwa kipa Erick Johola kuweza kuokoa penalti sawa na Kigonya Mathias wa Azam FC lakini ni Yassin Mustapha aliweza kukosa penalti na kuifanya Azam kushinda penalti ya mwisho kupitia kwa Mudhathir Yahya.