Home Sports NYOTA HAWA WA YANGA KUIKOSA AZAM FC KESHO

NYOTA HAWA WA YANGA KUIKOSA AZAM FC KESHO

KUELEKEA katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi kesho Januari 10 kati ya Yanga dhidi ya Azam FC baadhi ya nyota wanatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi ambapo waliweza kulitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti mbele ya Simba.

Ni Salum Aboubakhari, ‘SureBoy’ ambaye ni kiungo na jezi yake ni namba 18 huyu anatarajiwa kuukosa mchezo.

Sababu ya Sure Boy kuukosa mchezo ni kuugua Malaria ambayo haikubaliki.

Pia Dennis Nkane naye anatarajiwa kuukosa mchezo kwa kuwa aliumia kwenye mchezo dhidi ya KMKM kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.

Razack Siwa, Kocha wa Makipa wa Yanga amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wapo ambao watakosekana na wapo ambao watakuja.

“Wapo wachezaji ambao watakosekana hilo lisiwape shida pia wapo wachezaji ambao watakuja, hatuna mashaka tutakuwa na mchezo mzuri hivyo mashabiki msiwe na hofu,”.

Previous articlePABLO:TUMEAMUA KUWAPA FURAHA MASHABIKI WETU
Next articleSAIDO AFUATWA NA WAARABU BURUNDI