Home Sports RATIBA YA LIGI KUU BARA

RATIBA YA LIGI KUU BARA

LEO Desemba 28 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kuchanja mbunga ambapo timu nne zinatarajiwa kushuka uwanjani kusaka pointi tatu.

Ni Coastal Union ikiwa imetoka kushinda mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City itasaka pointi mbele ya Mtibwa Sugar iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa utachezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.

Pia KMC itashuka Uwanja wa Azam Complex ambapo itamenyana na Ruvu Shooting kwenye msako wa pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba jana Desemba 27 kulikuwa na mechi ambazo zilichezwa na baada ya dakika 90 mambo yalikuwa namna hii:-

Geita Gold 1-1 Mbeya Kwanza Uwanja wa Nyankumbu.

Polisi Tanzania 0-0 Mbeya City, Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Previous articleKIUNGO MPYA YANGA KUKUNJA MILIONI 158
Next articleSIMBA KUNDI MOJA NA RS BERKANE KOMBE LA SHIRIKISHO