Home Sports MSHAMBULIAJI YANGA AMALIZANA NA DODOMA JIJI

MSHAMBULIAJI YANGA AMALIZANA NA DODOMA JIJI

BAADA ya kuvunja mkataba na mabosi wake wa zamani Yanga sasa Wazir Junior ni mali ya Dodoma Jiji.

Dili lake ni la mwaka mmoja na miezi sita kwa ajili ya kuweza kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata.

Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuanza kuonekana kwenye kikosi hicho kwa msimu huu wa 2021/22 ndani ya uzi wa Dodoma Jiji.

Kwa mujibu wa katibu wa Dodoma Jiji, Johnson Fortunatus amesema kuwa wamefanya hivyo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye timu hiyo.

“Ujio wake ndani ya Dodoma Jiji ni kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chetu na tunaamini kwamba tutafanya vizuri,”.

Jr amewahi kucheza ndani ya Mbeya City, Azam FC na Mbao FC.

Previous articleNYOTA WATATU WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA
Next articleWAWA,SAKHO HATMA YAO MIKONONI MWA PABLO