WAWA,SAKHO HATMA YAO MIKONONI MWA PABLO

HATMA ya kiungo mshambuliaji, Ousmane Sakho na beki Pascal Wawa na wenzao watatu wanaotajwa kuweza kuachwa kwenye usajili wa dirisha dogo itajulikana hivi karibuni kwa kuwa tayari Kocha Mkuu, Pablo Franco ameshakabidhi ripoti ya usajili.

 

Nyota wengine wanaotajwa kuweza kuachwa katika timu hiyo ni kiungo, Duncan Nyoni, kipa Jeremiah Kisubi, na kiungo mkabaji Abdoulswamad Kassim na kufikisha jumla ya idadi ya nyota watano ambao wapo kwenye hatihati ya kuondoka hapo kwa mkopo ama kuachwa kabisa.

 

Taarifa zimeeleza kuwa usajili wa Simba unategemea ripoti ya Pablo hivyo yale maelekezo ambayo atayatoa kiujumla yatafanyiwa kazi na viongozi wa Simba.

“Ripoti ndiyo itakayoamua wachezaji wa kuachwa na kusajili wapya baada ya tetesi nyingi za usajili kusambaa katika vyombo vya habari,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mwenyekiti wa Simba, Murtanza Mangungu hivi karibuni aliweka wazi kwamba watafanya usajili makini kulingana na mapendekezo ya mwalimu.

“Usajili tutafanya lakini ni kulingana na ripoti ya mwalimu itakavyoelekeza hivyo mashabiki wa Simba ni muhimu kuwa na subira kila kitu kitakuwa sawa,”.