NYOTA WATATU WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA

Bruce Kangwa, Nivere Tigere na Prince Dube wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi kuu Bara ujao dhidi ya Simba.

Nyota hao wote watatu wameanza mazoezi katika timu ya taifa ya Zimbabwe.

Simba na Azam FC zinatarajiwa kumenyana Januari Mosi 2022 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi mwaka mpya.

Nyota hao wote wapo nchini Zimbabwe tayari kwa ajili ya maandalizi ya AFCON.

Unatarajiwa kuwa mchezo wenye ushindani kwa kuwa timu zote mbili zimetoka kushinda mechi zao zilizopita.

Azam FC ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting na Simba ilishinda mabao 4-1 dhidi ya KMC.