Home Sports SENZO:HATUNA PRESHA NA SIMBA

SENZO:HATUNA PRESHA NA SIMBA

SENZO Mbatha, Mtendaji Mkuu wa Yanga amebainisha kwamba hawana presha na watani zao wa jadi Simba kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11.

Kesho mchezo huo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa unatarajiwa kuchezwa.

Mbatha amesema kuwa wanatambua kuhusu mchezo huo kwa kuwa upo kwenye ratiba hivyo watafanya maandalizi mazuri ili kupata ushindi.

“Ipo wazi kwa muda mrefu kwamba lazima tutakutana na Simba kwenye mechi ya ligi hivyo hakuna presha kuelekea mchezo huo, kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yake ni kama ilivyo kwenye michezo mingine.

“Mwendo ambao tunakwenda nao nina amini kwamba mashabiki wanaona hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka juu ya uwezo wa wachezaji wetu ambao wapo kwani kila mmoja anafanya kazi kwa umakini katika kutimiza majukumu yake,” amesema Mbatha.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 19 inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 17 zote zikiwa zimecheza mechi saba.

Previous articleMKWANJA WAWEKWA WA KUTOSHA KWA SIMBA KISA YANGA
Next articleMUGALU NA LWANGA WAONDOLEWA KWENYE MIPANGO YA PABLO