Home Sports YANGA, AZAM ZAINGILIA USAJILI WA SIMBA

YANGA, AZAM ZAINGILIA USAJILI WA SIMBA

 

WAKATI Simba SC ikitajwa kuwa karibu zaidi kuipata saini ya mshambuliaji wa Zanaco FC, Moses Phiri, imeelezwa kuwa Yanga na Azam zimeingilia dili hilo.


Mshambuliaji huyo ambaye aliwatesa
Yanga katika mchezo wa kirafiki katika kilele cha Wiki ya Mwananchi, ameonekana kuwa lulu kwa timu mbalimbali hapa nchini.

 

Hivi karibuni, ilielezwa kwamba, Phiri usajili wake ndani ya Simba unakuja baada ya timu hiyo kuwa na mpango wa kuachana na nyota mmoja wa kimataifa, Duncan
Nyoni raia wa Malawi na nafasi yake
kuchukuliwa na Mzambia huyo.


Chanzo chetu kutoka Zambia kilicho
karibu na mchezaji huyo, kimeliambia Spoti Xtra, kwamba, baada ya Simba kuonekana kuwa siriazi katika usajili wa nyota huyo, Yanga na Azam nao wameibuka.


“Unajua Phiri awali alikuwa anatakiwa na
Yanga, lakini alishindwa kujiunga nao kwa sababu viongozi wa Yanga walitaka kumpa mkataba wa awali, kisha asajiliwe baadaye kitendo ambacho mwenyewe alikataa.

“Sababu kubwa ya kukataa mwanzo ni kwamba aliwaambia hawezi kusaini mkataba huo kwani inaweza kutokea timu na dau kubwa zaidi ikamfunga kusaini.

 

“Akawaambia wasubiri mpaka dirisha dogo ambapo mkataba wake utakuwa umebaki muda kidogo kabla ya kumalizika ili wafanye dili. Usajili wenyewe wa dirisha dogo huko Tanzania unakaribia, hivyo lolote linaweza kutokea.


“Mbali na Yanga, hivi karibuni baada
ya kutoka taarifa kwamba Simba wanamtaka Phiri, kuna kiongozi mmoja
wa Azam alimpigia simu mchezaji na
kumuuliza kama kweli anakwenda Simba, akamwambia bado. Hivyo nao
wanamtaka,” kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa mchezaji mwenyewe
kuhusiana na hilo, alisema: “Ni kweli timu tatu za Tanzania zinanitaka, chochote
kikitokea nitakujulisha lakini mpaka sasa
bado hakuna sehemu niliyosaini.”

Previous articleAZAM YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR
Next articleMWAMUZI AGOMA KUCHEZESHA DABI,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO