>

AZAM YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kuelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina inatarajiwa kumenyana na Kagera Sugar, Desemba 12.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku na utakuwa mubashara Azam TV.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kikosi kinaendelea na mazoezi.

“Kila mchezo kwetu ni muhimu na kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu kwa kuwa ni mchezo wa ligi hivyo lazima tufanye vizuri.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu na tunatambua kwamba wana timu imara lakini hatuna mashaka tunahitaji pointi tatu muhimu,”

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya 7 na pointi zake ni 10 baada ya kucheza mechi 7 Kagera Sugar ipo nafasi ya 12 na pointi zake ni 8.