NI dakika nyingine tena 90 zitakazoamua hatma ya Tanzania kupata mwakilishi kimataifa kama msimu uliopita wa Klabu Bingwa Afrika walivyokuwepo Simba na kutinga Robo fainali.
Kwanza kabisa Simba wanatakiwa kusahau matokeo yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam kuwa hata Red Arrows wanaweza kupata matokeo kama waliyopata Simba kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani.
Pia wakumbuke lile jinamizi la Jwaneng Galaxy jijini Dar es Salaam lililowakumba na kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Waswana.
Simba wanatakiwa kucheza kwa mbinu na kuendeleza ukubwa dhidi ya Red Arrows nikimaanisha angalau waanze kwa kushambulia zaidi ili kuwaondolea comfortability Red Arrows ya kuona wanawaweza Simba na Simba wacheze kwa malengo wacheze dakika 20 za mwanzo kwa kufunguka na kupata bao la mapema.
Wanasema njia nzuri ya kujilinda ni kumshambulia mpinzani wako naona kocha Pablo Franco huwa ni muumini mzuri wa kukabia juu akiwaweka Dilunga, Morisson & Bwalya nyuma ya mshambuliaji mmoja.
Hawa ni wazuri sana katika kuvuruga mipango ya timu pinzani hasa kupanga mashambulizi ya kuanzia nyuma.
Red Arrows wanachotakiwa kufanya na wao ni kuwavuruga Simba kwa kudominate mchezo muda mwingi na kupata mabao angalau mawili mapema kipindi cha kwanza hili linaweza kuwarudisha mchezoni kuwapa matumaini ya kuwaondosha Simba kwenye mashindano hayo muhimu kwa timu zote mbili.
Nafikiri ubora wa Simba ulikuwa kwa upande wa benchi la ufundi ndio lilikuwa na mbinu nzuri ya kuwafanya Simba wapate mabao ya mapema pia uwezo binafsi wa Bernard Morisson uliamua mchezo na kuwanufaisha Simba.
Nadhani madhaifu ya Simba ni timu haichezi kitimu zaidi inabebwa na uwezo binafsi wa mchezaji mmoja kama alivyofanya Morisson Dar es Salaam napia Kibu Denis Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kule CCM kirumba Mwanza nadhani wakikutana na timu itakayokuja na Plan ya kuwazuia hao key players Simba wanaweza kupata wakati mgumu.
Red Arrows waliathiriwa zaidi na uwanja kujaa maji na wao wakiendelea kuposess mipira kwa kupiga pasi,ila nawaona imara kwenye kufanya mashambulizi kupitia pembeni kwa Felix Bulaya huyu ni wing Midfielder Versatile Player ananyumbulika ipasavyo akishirikiana na Kayembe kujaribu kuisukuma timu isogee mbele.
Madhaifu ya Red Arrows ni kisaikolojia walikuwa wanatoka mchezoni kirahisi sana kwa maamuzi ya refa walikuwa wakicheza rafu nyingi sana zinazoonyesha wameghazabika sana hii ni hatari sana kama mchezo wa leo nao wataingia kwa kupanic inaweza waathiri zaidi ya mwanzo.
Tusubiri na tuone ni leo Desemba 5 mchezo huu unatarajiwa kuchezwa nchini Zambia. Simba ni muhimu kuwaheshimu Red Arrows kwani ile picha dhidi ya Jwaneg Galaxy bado haijisha kwenye kumbukumbu za mashabiki.