Home Sports MATAIFA MANNE YAIMALIZA RED ARROWS

MATAIFA MANNE YAIMALIZA RED ARROWS

MATAIFA manne yalitosha kuwatuliza Wazambia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Simba 3-0 Red Arrows.

Ni Bernard Morrison kutoka Ghana aliweza kuwapa tabu Wazambia kwa kuwa alihusika kwenye mabao yote matatu, alifunga mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Meddie Kagere raia wa Rwanda aliweza kufunga bao moja kwa pasi ya Morrison ilikuwa dakika ya 19 na pasi hiyo ikumbukwe kwamba Morrison aliipokea kutoka kwenye miguu ya Sadio Kanoute.

Kanoute yeye ni raia wa Senegal hivyo aliweza kufanya muunganiko wa mataifa matatu katika kusaka bao la pili kwa kuwa pasi ilianzia kwenye miguu ya nyota huyo aliyetoka Senegal kisha ikatua kwa miguu ya Morrison wa Ghana aliyempa pasi ya mwisho Kagere wa Rwanda.

Mohamed Hussein ambaye ni mzawa yeye alikamilisha hesabu ya taifa la nne ambapo alitoa pasi ya bao kwa mpira wake aliorusha dakika ya 77 ukakutana na Morrison aliyepachika bao la tatu lililopeleka kilio kwa Red Arrows.

Previous articleKIUNGO SIMBA AKUBALI KUSAINI YANGA
Next articleISHU YA USAJILI AZAM FC IPO HIVI