Home Sports AZAM FC WAMEKIWASHA HUKO,DUBE NDANI

AZAM FC WAMEKIWASHA HUKO,DUBE NDANI

BAADA ya kumaliza kazi ya kusepa na pointi tatu muhimu mbele ya Mtibwa Sugar, matajiri wa Dar hesabu zao kwa sasa ni kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wao uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar ilikuwa ni Novemba 30, Uwanja wa Azam Complex ambapo mtupiaji alikuwa ni Idris Mbombo kwa pasi ya Bruce Kangwa.

Jana, Desemba 2 kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kiliaza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na Kagera Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex na utachezwa saa 1:00 usiku itakuwa ni Desemba 9.

Miongoni mwa nyota ambao wamerejea na kuanza mazoezi ni pamoja na mshambuliaji wao namba moja Prince Dube ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo na alipofanyiwa matibabu alipaswa kukaa nje kwa muda ili kuweza kurejea kwenye hali yake.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na hali ya dube ipo sawa

 

Previous articleMZEE WA KUCHETUA ATUMA UJUMBE KWA WAZAMBIA
Next articleANACHOKIWAZA MUKOKO JUU YA SIMBA KIPO NAMNA HII