Home Sports YANGA HAWATAKI KABISA DENI WAMALIZANA NA MORRISON

YANGA HAWATAKI KABISA DENI WAMALIZANA NA MORRISON

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa tayari umemlipa kiungo wao zamani Mghana, Bernard Morrison faini ya Sh
12Mil kutoka Mahakama ya 
Usuluhishi wa Michezo ‘CAS’ huku ukiwataka mashabiki wa timu hiyo kupotezea majibu ya hukumu hiyo.


Hiyo ikiwa ni siku chache tangu 
CAS itangaze hukumu ya Morisson na Yanga ambayo ilishindwa huku ikitakiwa kumlipa kitita cha Swis 5,000 (Sh12,396,787).


Katika hukumu hiyo iliyokuwa 
na kurasa 29 imeeleza kuwa ushahidi uliotolewa na Yanga juu ya mkataba mpya uliotolewa na klabu hiyo ulikuwa na makosa mengi na kushindwa kuwa na ushahidi wa kutosha kama ulisainiwa na Morrison.

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa, katika hukumu kuna maamuzi mawili kushinda na kushindwa, hivyo Wanayanga wasahau hayo na badala yake kurejesha nguvu katika Ligi Kuu Bara.


“Wao (Simba) wametushinda CAS, basi 
na sisi Yanga tunatakiwa kuwashinda uwanjani kwa matokeo mazuri tutakapokutana nao Desemba 11, mwaka huu katika mchezo wa ligi.


“Tulikuwa tuna matarajio makubwa ya 
kushinda kesi hii CAS, hiyo ndiyo sababu ya kutumia gharama kubwa ya kukata rufaa CAS baada ya maamuzi ya utata TFF.


“Hivyo Wanayanga tunatakiwa 
kuungana kwa pamoja katika kuisapoti timu yetu katika michezo ya ligi na kikubwa kuchukua ubingwa huo katika msimu huu na Kombe la FA,” alisema Mwakalebela.

Previous articleNAMNA SIMBA WALIVYOICHAPA 3-0 RED ARROWS KWA MKAPA
Next articleMASAU BWIRE AIBUKA ABAMBIKIWA ISHU YA USHINDI WA SIMBA KIMATAIFA