Home Sports MASAU BWIRE AIBUKA ABAMBIKIWA ISHU YA USHINDI WA SIMBA KIMATAIFA

MASAU BWIRE AIBUKA ABAMBIKIWA ISHU YA USHINDI WA SIMBA KIMATAIFA

BAADA ya Simba jana Novemba 28 kushinda mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows huku nyota wa mchezo akiwa ni Bernard Morrison kuna ujumbe kutoka twiter ulisambaa kwa kasi kubwa.

Ujumbe huo ulionekana kuandikwa kwa jina la Masau Bwire ambaye ni Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ambapo alionekana kuwapa pongezi Simba kwa ushindi huku akimpongeza mchezaji Morrison.

Ulikuwa namna hii:-

Kuhusu ujumbe huo Bwire ameandika namna hii:-Hii nimebambikwa, sijaisema. Hivi kwa nini watu wanafanya hivi? Kwa nini wasitumie majina yao kwenye taarifa zao?. Sina maneno ya kipuuzi kukera wengine, namuomba Mungu aendelee kunipa hekima na busara maisha yangu yote katika mpira.

“Hata kwa bahati mbaya, isitokee kusema upuuzi wa kukera na kuhudhi wengine. Puuzeni andiko hilo, ni mpuuzi mmoja kaamua kujaribu kunigombanisha na watu kwa sababu anazozijua yeye,”.

Previous articleYANGA HAWATAKI KABISA DENI WAMALIZANA NA MORRISON
Next articleALIYEMTUNGUA BAO LA MBALI MANULA AREJEA KAZINI