ZIDANE AGOMEA DILI LA MANCHESTER UNITED

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Manchester United inamtaka Kocha Zinedine Zidane raia wa Ufaransa kutua klabu hapo kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kufuatia kufungashiwa virago kwa Ole Gunar Solskjaer lakini kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, amesema hana mpango wa kwenda Old Trafford.

 

Solskjaer alitimuliwa na Unites Jumapili baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Watford na kabla ya hapo hakuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo klabuni hapo hasa baada ya kipigo cha bao 5-0 dhidi ya Liverpool na kile cha bao 2-0 dhidi ya Man City.

 

Zidane hana timu tangu aondoke Real Madrid mwezi Mei mwaka huu na ameshinda mataji matatu mfululizo ya ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia mwaka 2016.

 

Baada ya kuondoka mara ya kwanza mwaka 2018, airejea mwaka mmoja baadae na kushinda taji la ligi kuu La Liga na kombe la Hispania la Super Cup mwaka 2020.

 

Chanzo hicho hicho kimesema kuwa kiungo huyo gwiji wa Ufaransa na Real Madris, ambaye hana timu sasa, hana mpango wa kujiunga na United kwa sasa kwa sababu ya Lugha ya Kiingereza na kwamba mkewe hataki kuishi Uingereza.

 

Zidane amekuwa akihusishwa na timu ya taifa ya Ufaransa na Klabu ya Paris St-Germain (PSG), na angependelea kuchangamkia nafasi za kuongoza timu hizo, fursa ikitokea.