GSM WASAINI DILI LA KUIDHAMINI LIGI KUU BARA

KAMPUNI ya GSM leo Novemba 23 imeingia mkataba wa udhamini wa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Mkataba huo unathamani ya bilioni mbili pointi moja,(2.1) ambao ni wa muda wa miaka miwili kwa ajili ya kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Masuala ya Uwekezaji ndani ya GSM amesema kuwa malengo ya uwekezaji huo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuinua mpira.

“Mkataba tulioingia nao ni wa miaka miwili una thamani ya bilioni mbili pointi moja kwa ajili ya Ligi Kuu Bara,utazihusisha timu zote ambazo zinashiriki ligi,” amesema.

Kwa upande wa TFF, Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani amesema kuwa watasimamia kwenye matumizi ya fedha hizo kwa kila klabu ili kuona namna ambavyo zitatumika.