Home Sports MORRISON AWASHUKURU YANGA

MORRISON AWASHUKURU YANGA

BAADA ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo,(CAS) kutoa maamuzi kuhusu kesi ya kiungo Bernard Morrison ambaye ilikuwa ni utata kuhusu mkataba wake na mabosi wake wa zamani Yanga mchezaji huyo ameandika ujumbe wa kushukuru.

Jana Novemba 22 CAS ilitoa hukumu kwa kueleza kuwa imetupilia mbali rufaa ya kesi iliyokatwa na Yanga kuhusu dili la mkataba wa miaka miwili ambayo walisema Yanga wamempa mchezaji Morrison ambayo iliwasilishwa Agosti 12,2020 hivyo kwa sasa mchezaji huyo yupo huru kuitumikia Simba.

Mchezaji huyo mzee wa kuchetua ameandika ujumbe wa kushukuru kwenye ukurasa wa Instagram namna hii:-

Hapa ni mwanzo na mwisho wa kila kitu hakuna ambacho kinachokuwa muda wote.Tulikuwa na muda wa kusubiri katika kipindi labda ilikuwa ni muda mzuri ama mbaya lakini mwisho wa siku kila kitu kimekuwa wazi

Ilikuwa ni suala la muda na kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea nilikuwa nahitaji kila mmoja ajue kwamba nilikuwa ndani ya Yanga kwa bahati na ninaheshimu fursa ambayo walinipa na kuweza kuvaa uzi wao katika ardhi ya Tanzania na namna ambavyo niliishi nao.

Hakuna ambaye alikuwa anajua kuhusu uwezo wangu Tanzania mpaka pale Luc Eymael alipoamua kunipa nafasi ya kuweza kucheza hapa nakushukuru mwalimu kwa kila kitu na kuweza kuniamini na kunifanya niwe kama nilivyo sasa.

Kule kwetu Ghana kuna msemo kwamba daktari mbaya ambaye anakuangalia wewe mpaka pale daktari mzuri atakapokuja ni lazima umuheshimu hata kama alikuwa ni mbaya alikufanya wewe ukaishi kwa muda huo mpaka pale mzuri alipokuja.

Kwangu mimi hii ni rasmi kwamba nasema asante Yanga na kila mmoja ambaye alinifanya nikaweza kutabasamu na kunipenda pia nilipokuwa ndani ya Yanga bila kuwasahau mashabiki namna ambavyo walikuwa wakinipa upendo.

Hakuna ambacho unakipokea ikiwa hujakipanda,

 

Previous articleAJIBU YAMEMKUTA SIMBA CHINI YA PABLO
Next articleGSM WASAINI DILI LA KUIDHAMINI LIGI KUU BARA