AJIBU YAMEMKUTA SIMBA CHINI YA PABLO

KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, hakuweza kumtumia kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Mchezo wake wa kwanza kukaa benchi mbele ya Ruvu Shooting alishuhudia timu yake ikishinda mabao 3-1 ikiwa ni ushindi mkubwa kwa Simba msimu wa 2021/22.


Alifanya kazi kwa kushirikiana na wasaidizi wake wawili ambao ni
Thiery Hitimana na Selemani Matola.

Kwa sasa Ajibu anaendelea vizuri baada ya kuwa chini ya uangalizi mkubwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu aliweka wazi kuwa Ajibu aliumia baada ya kujikwaa katika mazoezi Uwanja wa Boko Veteran.