>

MASTAA WA ENGLAND WATAWALA TUZO ZA FIFA

MAJINA ya mastaa ambao wanacheza ndani ya Ligi Kuu England wameweza kupenya majina yao kwenye suala la kuwania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA katika orodha ya wachezaji 11.

Ni Mohamed Salah raia wa Misri anayecheza ndani ya Liverpool,Kevin De Bruyne mali ya Manchester City na Cristiano Ronaldo mshambuliaji wa Manchester United pia yupo N’Golo Kante na Jorginho hawa wote ni mali ya Chelsea na mastaa wengine ambao wapo ni pamoja na Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe hawa wapo PSG.

Kwa namna ambavyo tuzo hizo zipo inaonekana kwamba Ligi Kuu England ni naba moja kwa timu ambazo zimetoa wachezaji wengi kuingia kwenye mchakato wa kuwania tuzo hizo za FIFA.

Pia yupo mshindi wa tuzo hiyo mwaka jana, Robert Lewandowski, Erling Haaland pamoja na mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema na tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Januari 7.

Ukiweka kando wachezaji kutoka Ligi Kuu England hata makocha wengi waliopenya kwenye orodha wamo ikiwa ni pamoja na Pep Guardiola anayeinoa Manchester City,Thomas Tuchel anayeinoa Chelsea pamoja na Antonio Conte ambaye kwa sasa yupo ndani ya Tottenham