BENZEMA APIGWA FAINI NA HUKUMU

MSHAMBULIAJI Real Madrid, Karim Benzema amepatikana na hatia katika kosa la kumtishia mchezaji mwenzake wa zamani kwenye timu ya taifa ya Ufaransa Mathieu Valbuena.

Inaelezwa kuwa Benzema aliweza kumuingiza kwenye mtego mchezaji huyo kuhusu masuala ya video ya udhalilishaji jambo ambalo lilimfanya aweze kuripoti Polisi.

Kwa kosa hilo Benzema atatumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya Mahakama ya Versailles kumkuta na hatia pamoja na faini ya Euro 63,000.

Mwanasheria wa Benzema,amesema kuwa mchezaji huyo atakata rufaa kuhusu maamuzi hayo.

Benzema ambaye alifanya vitendo hivyo hakuwa mahakamani wakati wa hukumu kwa kuwa alikuwa na majukumu kwenye timu yake ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Haya matokeo yaliyotoka hakuna namna ambayo tunaweza tukasema katika uhalisia hasa katika tukio lenyewe,” amesema mwanasheria Antoine Vey.