MWENDO WA AZAM FC BAADA YA MECHI 6

AZAM FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina baada ya kucheza mechi 6 za Ligi Kuu Bara imekusanya pointi 7 msimu wa 2021/22.

Ipo nafasi ya 10 na imetupia mabao matano huku ikiwa imeruhusu mabao ya kufungwa 7.

Haijawa kwenye mwendo mzuri kwa mechi hizi za mwanzo kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa ni kushindwa kutumia nafasi ambazo zimekuwa zikitengenezwa na wachezaji hao kwenye mechi ambazo wanacheza.

Imeweza kushinda mechi mbili ambazo ni dakika 180 huku ikiwa imepoteza mechi tatu na kuambulia sare moja pekee ndani ya uwanja.

Vivier Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wamekuwa wakitengeneza nafasi ila wanashindwa kuzitumia jambo ambalo wanalifanyia kazi.

“Wachezaji wamekuwa wakitengeneza nafasi lakini wanashindwa kuzitumia, kwenye mpira nafasi moja ukitengeneza hauwezi kuipata tena wakati mwingine hivyo hilo ni jambo ambalo tunalifanyia kazi,”.

Mchezo wake ujao ni dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Novemba 30 itakuwa Uwanja wa Azam Complex.