Home Sports MANE ATAKA MKWANJA KAMA WA SALAH

MANE ATAKA MKWANJA KAMA WA SALAH

WINGA matata ndani ya kikosi cha Liverpool, Sadio Mane imeripotiwa kwamba anataka mshahara kama anaopewa mshambuliaji matata ndani ya kikosi hicho Mohamed Salah.

Kiwango cha Mane msimu huu wa 2021/22 kimezidi kuwa imara akiwa ametupia mabao saba kwenye mechi 12 ambazo amecheza mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu England.

Mkwanja ambao anakuja kwa wiki Salah raia wa Misri ni Euro 200,000 na katika mkataba wake mpya Salah anataka kulipwa Euro 400,000 kwa wiki huku Mane raia wa Senegal yeye kwa wiki anakunja Euro 100,000 halafu hakuna mazungumzo ya mkataba mpya.

Ripoti zinaonyesha kwamba Mane anataka mshahara mpya lakini sasa inaelezwa kuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp hajafanya lolote mpaka sasa kwenye mikataba ya mastaa hao na inatajwa kuwa mmoja kati yao anaweza asipewe kabisa mkataba.

Previous articleMAYELE HATARI YAKE NI KILA BAADA YA DAKIKA 399
Next articleMWENDO WA AZAM FC BAADA YA MECHI 6