NAMUNGO HAWANA DOGO,WATUMA UJUMBE YANGA

UONGOZI wa Namungo umebainisha kwamba malengo makubwa ambayo wanayo ni kuweza kushinda mechi zao zote zilizopo mbele yao ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Yanga.

Leo Novemba 20, Namungo FC itawakaribisha Yanga kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ilulu majira ya saa 10:00 jioni.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Namungo FC, Omar Kaya amesema kuwa hesabu kubwa za timu hiyo ni kupata matokeo mazuri kwenye kila mchezo.

“Tunawachezaji wazuri na wenye uwezo hivyo kwa mechi ambazo zimepita hapo nina amini kwamba wapo wengine bado hawajapata nafasi za kucheza na wataonekana wakiwa na uzi wa Namungo.

“Wachezaji wote ambao tumewasajili ni pendekezo la benchi la ufundi hivyo mashabiki tuwe pamoja kwa ajili ya timu yetu na tunategemea tutafikia malengo yetu ya kupata pointi tatu kwenye mechi tutakazocheza,”

Namungo ikiwa na pointi zake tano ipo nafasi ya 12 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 15 zote zikiwa zimecheza mechi tano.

Timu hiyo imetupia jumla ya mabao manne ambapo ni wachezaji wawili wamefunga mabao hayo Shiza Kichuya na Relliats Lusajo wenye mabao mawilimawili kila mmoja.