WACHEZAJI WA AZAM FC WAREJEA KAMBINI TAYARI KWA KAZI

WACHEZAJI wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina  ambao walikuwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars tayari wamejiunga na wengine kambini.Ilikuwa ni jana Novemba 16, siku ya Jumanne walianza mazoezi kuivutia kasi KMC kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.

Nyota hao ni pamoja na Idd Seleman, Edward Manyama na Lusajo Mwaikenda walianza mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine katika Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo wao dhidi ya KMC unatarajiwa kuchezwa Novemba 21,Uwanja wa Uhuru.

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi 15 kibindoni ina pointi mbili huku Azam FC yenyewe ikiwa nafasi ya 8 na pointi 7.