>

SIMBA KUIBUKIA MWANZA LEO KUWAFUATA RUVU SHOOTING

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Pablo Franco leo Novemba 17 kinatarajiwa kukwea pupa kuelekea Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Ijumaa ya Novemba 19 saa 10:00 jioni Uwanja wa CCM Kirumba.

Tayari Franco raia wa Hispania aliyetambulishwa Novemba 6 kuchukua mikoba ya Didier Gomes ameanza majukumu ya kuwafundisha wachezaji wa Simba.

Anafanya kazi kwa ushirikiano na Seleman Matola na Hitimana Thiery ambao hawa ni makocha wasaidizi wa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.