Home International CONTE:KUANZA NA SARE NI MWENDO MZURI

CONTE:KUANZA NA SARE NI MWENDO MZURI

Antonio Conte, Kocha Mkuu wa Tottenham amesema kuwa vijana wake wanahitaji muda zaidi kuweza kurejea kwenye ubora na kuonyesha kile ambacho wanacho ndani ya uwanja huku kuanza kwa sare ya bila kufungana akiamini kwamba ni mwendo mzuri wa kuanzia.

 

Mrithi huyo wa mikoba ya Nuno Espirito ambaye alifutwa kazi ndani ya timu hiyo kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo ndani ya Ligi Kuu England.

Katika mchezo wake wa kwanza katika Ligi Kuu England,  Conte alilazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Everton na kufanya timu hiyo ifikishe jumla ya mechi tatu mfululizo bila kushinda pia katika mchezo huo alishuhudia mchezajinwa Everton,  Mason Holgate akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+2.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba kwa namna ambavyo ameanza na alivyowaona wachezaji hao anaamini kwamba watafanya mambo makubwa hapo baadaye.

Mchezo wake wa pili itakuwa ni Novemba 21 ambapo atakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Leeds United.

Previous articleSIMULIZI YA ALIYETAKA KUFURUMUSHWA KISA ALIKUWA KIJIJINI
Next articlePABLO YUPO DAR TAYARI KUINOA SIMBA