>

HOWE KOCHA MPYA NEWCASTLE UNITED

KLABU ya Newcastle United imetaja jina la Eddie Howe kuwa mbadala wa Steve Bruce ambaye alifutwa kazi hapo hivyo kocha huyo wa zamani wa Bornemouth anatarajiwa kuanza kazi yake mpya na matajiri hao ndani ya Ligi Kuu England.

Howe hakuwa kwenye kazi baada ya kuondoka  Bournemouth  2020 anarejea kwenye majukumu mapya akiwa na timu mpya ambayo ina hesabu kali ikitumia Uwanja wa St James’ Park.

Newcastle awali walikuwa wanatajwa kumchukua kocha wa zamani wa  Arsenal ambaye kwa sasa anainoa Villarreal Unai Emery  ila alichagua kubaki ndani ya La Liga hakutaka kurudi kwenye Ligi Kuu England jambo ambalo liliwafanya mabosi hao wasiwe na chaguo juu yake.

Rekodi zinaonyesha kuwa Howe katika kazi ya ukocha amesimamia jumla ya mechi 545, ameshinda mechi 228, sare 114 na kichapo ilikuwa kwenye mechi 203.

Howe amesema kuwa ni jambo kubwa kwake kuweza kuwa kocha kwenye timu hiyo hata familia yake inafurahi kushusu hilo.

“Ni heshima kubwa kuja kuwa kocha hapa kwenye timu yenye historia kama  Newcastle United, ni siku kubwa kwangu na familia pia” amesema Howe,ambaye leo Jumanne atafanya mazoezi na timu hiyo kwa mara ya kwanza.