UJUMBE WA MORRISON HUU HAPA

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kuwa licha ya hali ngumu wanayokutana nayo mwanzoni mwa msimu huu, bado kikosi hicho kina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba kwa sasa ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi tano za Ligi Kuu Bara.

Mchezo wake wa tano iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na mtupiaji alikuwa ni Meddie Kagere kwa pasi ya Mohamed Hussein.


Mambo yamekuwa tofauti na wengi ambavyo walifikiria kutokana na kuwa kwenye hali ya kusuasua jambo ambalo limekuwa liwapa tabu mashabiki pamoja na wachezaji kuwa kwenye presha.

Morrison amesema: “Ni kweli hatujawa na matokeo mazuri katika michezo yetu
iliyopita msimu huu kulinganisha 
na wapinzani wetu, lakini niwahakikishie kuwa bado tuna muda wa kubadilisha hili na kama wachezaji tunafanya kila jitihada kuhakikisha tunapambana kutetea kombe letu msimu huu licha ya upinzani mkubwa ambao tunatarajia kukutana nao kutoka kwa wapinzani wetu.”

Kinara wa Ligi Kuu Bara kwa sasa ni Yanga mwenye pointi 15 baada ya kucheza pia mechi tano ni ameshinda mechi zote kwa asilimia 100 na ushindi mkubwa ilikuwa ni wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting.