Home International SOLKJAER AWAPONGEZA WACHEZAJI WAKE KWA USHINDI

SOLKJAER AWAPONGEZA WACHEZAJI WAKE KWA USHINDI

OLE Gunnar Solskjaer,  Kocha Mkuu wa Manchester United amewapongeza wachezaji wake kwa mbinu na uwezo walioonyesha katika mchezo wao wa Ligi Kuu England na kushinda mabao 3-0 mbele ya Tottenham wakiwa ugenini.

 

Solskjaer aliwaongoza vijana wake katika mchezo huo mgumu wakiwa na kumbukizi mbaya ya kupokea kipigo cha udhalilishaji ambapo ni mabao 5-0 walifungwa na Liverpool wakiwa Uwanja wa Old Trafford jambo lililoongeza presha kwa timu hiyo.

Kurejea kwa Raphael Varane kulimpa unafuu Solskjaer ambaye alibadili mfumo na kutumia 3-4-3 akiwa ndani ya Uwanja wa Tottenham Hotspur pamoja na kuanza na Cristiano Ronaldo ambaye alipachika bao dakika ya 39 huku Edson Cavan akifunga dakika ya 64 na mkwaju wa mwisho ukijazwa kimiani na Marcus Rashford dakika ya 86.

Mbele ya mashabiki 60,356 ikiwa ugenini United ilisepa na pointi tatu mazima huku Ronaldo akichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa na Cristian Romero wa Spurs alipata nafasi ya kufunga lakini bao lake ilikuwa ni la kuotea kwa mujibj wa mwamuzi.

Previous articleMASTAA YANGA WAOGA MAMILIONI, SIMBA WANA JAMBO LAO
Next articleMAMBO 7 YALIWATOA SIMBA KWENYE RELI LIGI YA MABINGWA