MILTON Nienov, raia wa Brazil aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Simba kabla ya kuchimbishwa Oktoba 26 amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kusaini dili jipya ndani ya Yanga ikiwa watafikia makualiano mazuri.
Kocha huyo kwa sasa yupo huru baada ya mabosi wa timu hiyo kufikia uamuzi wa kuachana naye kutokana na kile waliochoeleza kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo kwa msimu mpya wa 2021/22.
Katika mechi tano ambazo aliweza kumnoa kipa namba moja Aishi Manula, kipa wake huyo aliokota nyavuni mabao manne ilikuwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba 0-1 Yanga,Simba 1-3 Jwaneng Galaxy huku mechi tatu hakufungwa ilikuwa Biashara United 0-0 Simba, Dodoma Jiji 0-1 Simba na Jwaneng Galaxy 0-2 Simba.
Nienov amesema kuwa hajafurahishwa kuona timu yake hiyo ya zamani kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa huku kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kikiwapotezea furaha ambayo walikuwa nayo.
“Ikiwa utahitaji kujua kuhusu hali yangu kwa sasa ni mbaya hasa baada ya kuona kwamba hatujafikia malengo lakini kwa kuwa yameshapita na sasa sipo ndani ya Simba ni jambo la kuangalia wakati ujao mambo yatakuaje.
“Kwa mfano nikapata ofa hapa Tanzania labda kutoka Yanga ama timu nyingine nitaweza kusaini lakini kwa kuzingatia manufaa ya makubaliano kwa pande zote mbili kwani ninaipenda Tanzania ni amani na upendo,” amesema Mbrazili huyo.