BECKHAM ALAMBA DILI LA MAANA

DAVID Beckham imeripotiwa kwamba amelamba dili la maana la ubalozi nchini Qatar kwa malipo ya pauni milioni 150 sawa na shilingi bilioni 475.

Dili hilo litamfanya staa huyo wa England kuweza kuuza sura kwenye Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Gwiji huyo alipigwa picha akiwa nchini humo mapema mwezi huu akitazama maeneo kadhaa ikiwemo viwanja vitakavyotumika kwenye Kombe la Dunia mwakani.

Kwa mujibu wa The Sun, Beckham mwenye miaka 46 atakuwa na kazi maalumu katika dili hilo litakalotangazwa rasmi mwezi ujao ambalo pia litahusika kutangaza utalii, utamaduni na vivutio vingine vya Qatar.

“David amekuwa akizungumza kuhusu nguvu ya soka katika mambo mbalimbali mazuri ya kijamii,” Ofisa Habari wa Beckham aliliambia The Sun.