Home Sports MASTAA WAWILI WA SIMBA KUIKOSA JWANENG GALAXY KESHO

MASTAA WAWILI WA SIMBA KUIKOSA JWANENG GALAXY KESHO

MASTAA wawili wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa kesho Oktoba 24 kuna hatihati ya kuwakosa mazima wapinzani wao Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni Chris Mugalu kipenzi cha Gomes kwenye suala la ushambuliaji huyu hajarejea kwenye utimamu baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma Simba ilishinda bao 1-0 lilipachikwa na Meddie Kagere na pasi ilitolewa na Mugalu na kuipa pointi tatu muhimu timu hiyo.

Mwingine ni Pape Osmane Sakho ambaye ni ingizo jipya ndani ya Simba naye pia alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi jambo ambalo limemfanya awe nje ya uwanja kwa muda.

Wote wawili walishindwa kucheza mchezo wa awali ambapo Simba ilishinda kwa mabao 2-0 Uwanja wa taifa Botswana jambo ambalo linawapa nguvu Simba kuweza kusonga mbele licha ya kwamba kazi kesho haitakuwa rahisi.

Kuhusu mchezo wa kesho, Hitimana Thiery, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji matokeo chanya ili kuweza kusonga mbele na kutinga hatua ya makundi.

Previous articleAZAM FC KAMILI KUWAVAA WAARABU WA MISRI LEO
Next articleJEMBE LA KAZI YANGA LAANZA MATIZI