Home Sports AZAM FC KAMILI KUWAVAA WAARABU WA MISRI LEO

AZAM FC KAMILI KUWAVAA WAARABU WA MISRI LEO

GEORGE Lwandamina, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa vijana wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Oktoba 23 dhidi ya Waarabu wa Misri, Pyramids FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa vijana wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huo muhimu katika mashindano ya kimataifa.

Huu ni mchezo wa Kombe la Shirikisho ikiwa ni mtoano na Azam FC wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bila kufungana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Leo saa 4:00 usiku Azam FC watakaribishwa na Pyramids FC ya Misri, Uwanja wa 30 June ambapo hesabu kubwa ni kwa timu hiyo kupata ushindi ili iweze kusonga mbele katika hatua ya makundi.

Katika mazoezi ya mwisho jana Oktoba 22, Balozi wa Tanzania nchini Misri, Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati aliwatembelea Azam FC na kupata nafasi ya kuzungumza na wachezaji na kuwatakia kila la kheri kuelekea mchezo huo.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo nchini Misri ni pamoja na kiungo mzawa Idd Seleman, ‘Nado’, kipa namba moja Mathias Kingonya, mshambuliaji Idrisa pamoja na Nicolas Wadada.

Previous articleKOCHA YANGA AIPA ONYO SIMBA
Next articleMASTAA WAWILI WA SIMBA KUIKOSA JWANENG GALAXY KESHO