>

KOCHA YANGA AIPA ONYO SIMBA

KOCHA wa Yanga Princes Mohamed Hussein, ‘Mmachinga’ amewapa onyo Simba kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Jwaneng Galaxy kwa kuwataka kucheza kwa kujilinda na kusaka ushindi mapema ili kuongeza hali ya kujiamini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa ushindi wa ugenini ni ishara mbaya kwamba hata wageni wao wanaweza kufunga wakiwa nyumbani hivyo ni lazima waongeze umakini mara dufu.

“Kushinda kwao ugenini ni ishara mbaya kwao pia kwamba kwenye mpira lolote linawezekana kinachotakiwa ni wao kuongeza umakini na kushinda katika dakika za mwanzo ili waongeze hali ya kujiamini.

“Imani ya Watanzania ni kubwa kwa Simba ila imani haiwapi ushindi mpaka pale watakapopambana bila kukata tamaa katika mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkali,” alisema.

Katika mchezo uliochezwa nchini Botswana Simba ilishinda mabao 2-0 yalifungwa na Taddeo Lwanga pamoja na John Bocco.