Home Sports JEMBE LA KAZI YANGA LAANZA MATIZI

JEMBE LA KAZI YANGA LAANZA MATIZI

MABINGWA wa kihistoria Yanga wameendelea na mazoezi kwa ajili ya kuivutia kasi Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 30.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imeendelea kujiweka sawa ambapo katika program wanazofanya kwa sasa ni pamoja na ile ya kuwa GYM kupiga matizi.

Mbali na mazoezi hayo pia jembe la kazi Said Ntibanzokiza ambalo lilikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu nalo pia limeanza kupiga matizi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea kwenye mechi zijazo.

Saido alikosekana kwenye mchezo wa ligi ule wa ufunguzi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba na Yanga ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar pia mchezo wa pili dhidi ya Geita Gold, wakati Yanga ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Hata kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba wakati Yanga ikishinda bao 1-0 na kusepa na taji la Ngao ya Jamii hakuwa kwenye kikosi ambacho kilianza.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wanahitaji kushinda kwenye mechi zao zote ili waweze kupata wanachohitaji kwa kuwa ni muhimu kupata pointi tatu.

“Kazi kubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi na tunajua kwamba haitakuwa rahisi lakini tupo tayari kwa ajili ya kuona tunafanikisha malengo yetu,” .

Previous articleMASTAA WAWILI WA SIMBA KUIKOSA JWANENG GALAXY KESHO
Next articleKMC WAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA NAMUNGO,ILULU