
MASHUJAA FC YATHIBITISHA KUACHANA NA WACHEZAJI WAKE WATATU
Klabu ya Mashujaa FC imethibitisha kuachana na wachezaji wake watatu ikiwa katika harakati za kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao. Wachezaji waliopewa mkono wa kwakheri jioni ya leo ni pamoja na Michael Masinda, Said Makapu na Shedrack Ntabindi.