VIDEO:BAADA YA USHINDI MBELE YA DODOMA,SIMBA KUMPA NGAMIA SAKHO
MZARAMO shabiki wa Simba ameweka wazi kwamba watampa zawadi kiungo Pape Skho tena ngamia huku akimwaga tambo baada ya timu hiyo kushinda mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkapa.
MZARAMO shabiki wa Simba ameweka wazi kwamba watampa zawadi kiungo Pape Skho tena ngamia huku akimwaga tambo baada ya timu hiyo kushinda mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkapa.
HUSSEIN Masalanga kipa wa Dodoma Jiji amesema kuwa wanacheza kwa kutumia mfumo wa mwalimu jambo ambalo limeonekana kuwafanya wawe bora, amedai kwamba penalti aliona ilikuwa ni nyepesi na iliweza kuwatoa nje ya mchezo kidogo kisha wakarudi kwenye ubora.
JAMIE Carragher amesema kuwa Klabu ya Everton ipo kwenye hatari ya kuwa katika Championship baada ya kukubali kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Spurs. Frank Lampard ambaye ni Kocha Mkuu wa Everton ameshuhudia timu hiyo ikipoteza katika mechi nne za Ligi Kuu England. Carragher ambaye ni mchambuzi ndani ya skysports amesema:”Ikiwa unaona timu inakuwa na…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne
UWANJA wa Mkapa Simba leo Machi 7 imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na ushindani mkubwa. Ni mabao ya Clatous Chama dakika ya 55 kwa mkwaju wa penalti na Meddie Kagere ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa akiwa ndani ya 18 ilikuwa dakika ya…
KIUNGO wa Polisi Tanzania ameweka wazi kwamba ana uwezo wa kucheza mbele ya Simba na Yanga huku akiwazungumzia Clatous Chama wa Simba pamoja na Khalid Aucho wa Yanga.
MSHAMBULIAJI namba moja ndani ya Yanga, Fiston Mayele akiwa ametupia mabao 10 kibindoni na pasi tatu za mabao amekabidhiwa zawadi ya ng’ombe mwingine tena baada ya ile ya kwanza kupewa alipokuwa Moro alipowatungua Mtibwa Sugar. Pia Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wengine wamepeleka samaki,madafu pamoja na zawadi mbalimbali.
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo Machi 7 ikiwa ni mzunguko wa 17. Ruvu Shooting itamenyana na Biashara United saa 8:00 mchana ni Uwanja wa Mabatini. KMC wao watamenyana na Coastal Union pale Azam Complex ngoma itakuwa saa 10:00 jioni. Simba SC itakuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Dodoma Jiji, saa 1:00 usiku.
BEKI wa Simba, Henock Inonga,Uwanja wa Mkapa alikuwa na biashara yake uwanjani mbele ya Biashara United kwenye mchezo wa ligi wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-0. Aliweza kutumia jumla ya dakika 65 na kutolewa kutokana na kupata maumivu lakini aliacha biashara ya msako wa pointi tatu ukiwa umekamilika kwa kuwa Simba ilikuwa tayari imeshatupia mabao…
KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Machi 7 kimewasili salama Dar baada ya kuanza safari mapema leo wakitokea Mwanza. Jana Machi 6,2022 Yanga ilikuwa kwenye msako wa pointi tatu na ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba. Bao la ushindi lilipachikwa…
BEKI bora katika kazi ngumu na chafu uwanjani Shomari Kapombe leo Machi 7,2022 anatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji. Kapombe aliumia katika mchezo uliopita mbele ya Biashara United na alikwama kuyeyusha dk 90 badala yake alitumia dk 30. Aliweza kutoa pasi mbili za mabao yaliyofungwa na Pape Sakho pamoja na Mzamiru Yassin….
BAADA ya kikosi cha Yanga kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Geita Gold Machi 6,2022 leo wanarejea Dar kikiwa na furushi la pointi kibindoni. Bao pekee la ushindi lilijazwa kimiani na Fiston Mayele dakika ya 1 na lilidumu mpaka kipyenga cha mwisho. Ushindi huo unaifanya Yanga iridium kujenga ngome kileleni ikiwa na pointi 45…
RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa walikuwa bora kipindi cha kwanza lakini wakashindwa kuzitumia nafasi ambazo walizipata. Usiku wa kuamkia leo ubao wa Uwanja wa Etihad ulisoma Manchester City 4-1 Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England. Ni mabao ya Kevin De Bruyne alitupia mawili dk 5 na 28 na Riyad…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
TIMU ya taifa ya Tanzania, U 17 ya Wanawake imeshinda mabao 7-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan,Zanzibar. Ni mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambao ulikuwa na ushindani mkubwa. Kipindi cha kwanza Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao manne na kipindi cha pili walifunga mabao matatu na kufanya hesabu kukamilika kwa…
Heritier Makambo, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa mchezo wao wa leo dhidi ya Geita Gold ulikuwa ni muhimu kwao kupata pointi tatu muhimu. Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanna wa CCM Kirumba umesoma Geita Gold 0-1 Yanga. Bao pekee la ushindi limefungwa na Fiston Mayele ilikuwa dakika ya kwanza na liliweza kudumu mpaka dakika…
UWANJA wa CCM Kirumba, ubao unasoma Geita Gold 0-1 Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Kasi ilianza kipindi cha kwanza ambapo Yanga walifanya majaribio mawili ambayo yalikuwa na hatari lakini ni moja liliweza kuzama nyavuni. Ni Fiston Mayele alipachika bao hilo mapema dakika ya kwanza kutokana na safu ya ulinzi ya Geita Gold…