Simba SC yasisitiza mshikamano kila wakati

UONGOZI wa Simba SC umebainisha kuwa mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuendelea kuwa na umoja nyakati zote ili kufikia malengo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kila shabiki anapaswa kutambua maendeleo yanajengwa kwa mshikamano nyakati zote.

Simba SC inapambania taji la ligi ambalo lipo mikononi mwa Yanga SC inayoongoza ligi ikiwa na pointi 18 sawa na mtani wake tofauti kwenye mabao yakufunga na kufungwa.

Ally amesema: “Mashabiki wa Simba SC wamekuwa na timu kila nyakati, hili ni jambo la msingi kuhakikisha kwamba tunapata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

“Kikubwa nikuona kwamba hatumuachi mtu nyuma kwenye mshikamano. Tuna mechi zenye ushindani na ngumu uwepo wa mashabiki unaongeza nguvu na kuwapa nguvu wachezaji kupambania ushindi,”.

Simba SC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili imekusanya pointi 18 baada ya mechi 6 msimu wa 2026/27 haijapoteza mchezo.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar