MORRISON ASIMULIA NAMNA ALIVYOFUNGA KIMATAIFA
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison mtupiaji wa bao lililoipa timu hiyo pointi moja amesema kuwa kwake ni furaha kufanya hivyo kwa ajili ya timu. Ilikuwa jana Februari 20 Morrison akitokea benchi wakati Simba ikiwa ipo nyuma kwa bao 1-0 aliweza kuingia na kufunga bao. Morisson aliingia dakika ya 64 akichukua nafasi ya Yusuph Mhilu…